Sakina Seventh-day Adventist Church
Sakina SDA Church Logo
Sakina SDA ChurchArusha, Tanzania
Kanisa la Waadventista Wasabato

Karibu Kanisani

Kutana na Mungu kwa njia ya maombi, nyimbo, kujifunza neno, sadaka na ushirika wa pamoja.

Ibada Kuu ya Sabato • Kila Jumamosi 09:00 AMTembeza Chini
SISI NI NANI

Waadventista Wasabato ni Akina Nani?

Sisi ni jamii ya waumini wa Kikristo ulimwenguni kote tunaomwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wetu. Tunaishi kwa imani katika Biblia Takatifu, tukitunza Sabato ya siku ya saba kama pumziko la kiroho, na tukiwa na tumaini kuu la kurudi kwa Kristo mara ya pili.

MWITO WETU

Kutangaza Injili ya Milele kwa Kila Mtu

Mwito wetu ni kutangaza injili ya milele ya Yesu Kristo katika muktadha wa ujumbe wa malaika watatu (Ufunuo 14:6-12) kwa watu wote, tukiwaongoza kumpokea Mwokozi na kuwaandaa kwa ajili ya kurudi Kwake upesi.

Neno la Mungu

Biblia Takatifu ndiyo ufunuo thabiti wa Mungu na kipimo kikuu cha maisha na imani yetu.

Wokovu kwa Neema

Tunaokolewa bure kwa neema ya Mungu kupitia imani katika kafara kamili ya Yesu Kristo.

Sabato ya Bwana

Tunashika siku ya saba (Jumamosi) kama Sabato takatifu ya pumziko na uumbaji.

Kurudi kwa Yesu

Tunaishi tukitazamia kwa furaha na matumaini ujio wa pili wa Yesu Kristo kwa utukufu.

HUDUMA YA KIDIJITALI

Shiriki Injili

Jumbe fupi na rahisi za Neno la Mungu — Posters za kuvutia, Reels, na Carousels zilizobuniwa tayari kwa ajili ya kushiriki kwenye WhatsApp Status na mitandao ya kijamii.

injili.sakinasdachurch.com • Bure kwa kila mtu
RATIBA YA IBADA

Vipindi vya Ibada na Ushirika

Karibu ushiriki nasi katika nyakati hizi za ibada, maombi na kujifunza neno la Mungu.

Kila Jumamosi

Ibada ya Sabato

Ibada ya Sabato09:00 AM - 06:30 PM
Kujifunza Biblia, mahubiri makuu, sifa, sadaka na ushirika wa pamoja wa Sabato.
Kila Jumatano

Maombi ya Juma

Kipindi cha Maombi05:00 - 06:00 PM
Maombi ya pamoja ya uombezi na kushukuru katikati ya juma.
Ijumaa Jioni

Kukaribisha Sabato

Ibada ya Vesper05:00 - 06:00 PM
Kuingia katika masaa matakatifu ya Sabato kwa nyimbo na neno.
MAHALI TULIPO

Sakina, Arusha, Tanzania

Fungua Google Maps